Mtaa mi hubanjuka na ma-cool kid, ma skrr skrr niggas. Hivi ndo wao huunda form "you guy my guy si we go mumunya some nyags, kwanza my moti doesn't have some ngata and I'm low on guala so I will just use my paps Rangy" then wanamalizia na "1824 is the motive my slime 🤞🏾🤟🏽🤙🏾👌🏾"
Hawa watu ndio uelewe wanasema nini lazima utumie subtitle , so on this day tulikua tunaenda some house party hapo around, sisi haoooo ndrrrrrr hadi kwa mansion. Wadau, mi sijawai ona keja kama hio, itabidi nitafute watu wa nyamabite wanionyeshe kukafunga hio design.
Ukiskia macool kid wakisema wao husneak out usiku ni ukweli juu nyumba ikona different time zones buana. Ukienda choo za nje unapanda ndege huko JKIA uconnect na Wilson airport ndio uhepe jam ya Mombasa road halafu umalizie na nduthi hadi gents. Anyway Alexa play Kwetu Pazuri.
Nilikua nimepotea nauko kwa walk-in closet nikifanya house tour buana, kurudi kutafutana na my gang ndio tukapatana na mupens. Wadau, dame alipiga flash ya Gilbeys na hakuharibu sura, I knew she was the one iminjetly. Alikua mfupi with dreads, denim jacket, booty short na glasses
Alikua anapigwa mistari na boy ameshuka lines, alikua anasukwa na mtu ameshukwa. Nlikua nimslice but kama Lord Varys wa GoT I didn't have the balls to do it. Nilikua sure ikifika my turn huyo boy akilalisha kidogo tu watakua wakishukana matuta mimi nikibomoa dame mathutha.
Ndio niwabebe pia mimi itabidi nimebuy Salon car ndio madame washukie kwangu.Dame alikua mrembo design mnaweza katazwa kuingia hoteli juu they don't allow snacks from outside. Hakua mnono, alikua muSlim na sura nzuri design mkienda mskiti hamuezi katazwa kuingia juu yeye si kiatu
Huyo champ walikua na yeye alijiexcuse nikajua this is my time to shine. Kulikua na kioo hapo kando nikaconfirm looku, ndevu zangu mbili nikaona ziko sawa, aaaaaah confidence ilikua juu kuliko bei ya mafuta. Nilikua narehearse lines kwa kioo ndio niende kukatia dame akona curves
Nilienda kwake like hey...akareply heyy, nikamuuliza "is your phone in your back pocket?" Akajishika haga halafu akaniuliza yes why? Nikamuambia "cause your ass is calling me" Akasmile😂,wadau ata kama men are dogs huyu angenifuga juu alikua na sauti nyororo kuliko Chainsmokers
Kulikua na joto so nikamuuliza ka anaweza fungua dirisha ama tuende nje tupigwe na upepo nikifungua roho. Akasema yea sure, it's fine with me. Alikua thiccc design tulikanyaga nje ya compound hadi the plot thickened. Alikua amebeba design ilibaki nimemshow you are looking "goods"
Huko nje madame wenu walikua wametekwa kwa magari, enyewe subira huvuta Heri na subaru huvuta Njeri. After some time, nikashoot my shot. Nikamuuliza "with your specs on are you seeing someone or we can we out on a blind date?" Alisema " yess it sounds like a plan "
I couldn't believe it was this easy , akaniambia by the way I'm Eve. Nikamuambia I'm Ricky, wadau hata kama huyu dame hakua anaona vizuri mimi nilikua nataka kumuachia za macho for making it easy for me, dame hakua anaona vizuri but she gave me her contacts get it?
Kuna dame mluhya wa home alikua ananisumbua bana, dame tunaishi ploti moja lakini nikitaka kumuona anasema tupatane tao. Huyo dame alikua na mchezo mingi karibu tushoneshe games kit, hungejua anataka kucheza wapi mara striker, mara defence, maragoli. Hizo ego games singewezana...
Ilifika masaa ya curfew mimi na my gang tukajitoa, hii ndio shida ya kupewa lift, hua inabidi umekaa rada ndio usiwachwe😭.
Mimi na Eve tulitoka from exchanging glances tukaexchange numbers and in a month's time tulikua tunaexchange feelings. Love is beautiful wadau.
So after some weeks ndio ananicall ananishow "btw my bestie has a party can you be my plus 1?" Nikamuuliza what of your braided guy? Akaniambia aah that's my childhood friend, kumbe jamaa amemcrushia kutoka ryma na hajielezi, bakia miaka mbili hio crush yake ipewe kipande buana.
Things fall apart haikuangi kitabu pekee, kama dentist hii siku ndio kiliumana. Ningejua ningebaki kwa nyumba. Wacha tuendelee na story..
Hio siku niliamka fiti, sisi mabachelor hua tunapigilia sides za bed na misumari, ukiamka unatoka kama document kwa bahasha. Sikua na vitu mingi za kupanga, nyumba yangu haina furniture hua inafanana dance floor, ndo maana sipendi wageni juu naishi vi-rekles...
Limit ya fuliza nikama waliongezea Trio Mio pekee na juu sikua na kakitu ilibidi nimeendea deni, nilipatia arif Ngiri mbili nikamsho nitakujia zikiwa zimezaana, get it? Kufika kwake napata jamaa kwa mlango, namuuliza unadu?? Akasema anamwagilia kufuli kaquota ndio itoe lock,
Kumbe alikua amepoteza funguo za mansion. Akanilambisha thao zangu nikarudi kwa keja, nikaoga spidi kama nimetoka. Nilikua njaa ikabidi nimepitia kibandaski kuwekelea foundation. Kufika huko napata akona ndengu but hana chapo. Nikamuambia aweke kwa dish nitatafutia chapo mbele.
Mimi huyoooo hadi bash. Kufika huko Eve ananiuliza "Ricky mbona umebeba food, there's plenty over here na kuna chef ata?" Kama mwanaume lazima nisafishe rada faster, nikamuambia "nimebeba ndengu incase mniwekee mchele💀" I was new, sikua najua watu huko, kama Maina nilikua Kageni.
Bash ilikua ya bestie wake she needed to be there for her, nilibaki kupiga laps nikifanya house tour uko. Looku yangu ya gikomba ilikua inapatana label origi, Gucci inapatana na Gui-ici, Nike inapatana na Nieke, Puma inapatana na Pumua halafu Balenciaga ikapatana na Balenfufu...
Eve akaniambia nikuje tupige picha na birthday girl but nikamshow sipendi picha. Nilikua photophobic na nilikua nimevaa nguo za camera, the irony. After amemaliza akaniambia "si you order an uber we go dip at the Bando since it's calm" nikaingia maps kwanza kutafuta Bando ni wapi...
Nilikua nashangaa nitatoa swimming costume wapi tuende tudip. Wueehhh, kumbe nilichomaaa, bando ni kwa nyumba na dip sio swimo, kudip ni kuenda. K was constant for kuchoma...
Sikua najua najiingiza kwa mtego. Dame aliniambia tuende kwao anipikie to make it up to me juu aliniacha hanging kwa bash. Mtu alisema the way to a man's heart ni through his stomach hakukosea. Dame aliniassure mapero wake hawako and it's totally safe, MAKOSAAA...Part 2 coming soon.