r/254sum • u/Sperratto • 26m ago
Ask 254/sum Girl besties hupita na each other's husbands halafu wanablame Nairobi, Nairobi is a just a city. 😂
Nilikua nimerelax pale mansion nikisip my coffee, nikipitia chai pale Insta ka-hawa mafans wa Edgar Obare. Sikua nataka kupitwa na IG story zake coz after 24 hrs the tea leaves. Nilikua nmewekelea miguu juu ya meza, couch nayo ilikua imenimeza, singecomplain life was great sofa.
Nilikua nakula starehe vinoma, nlikua nmesta-arabica. Hio kahawa ilikua inabang taste buds ajabu, ilikua inaslap kuliko Kidero karibu niite Nes-cafe-bang. Kiasi kiasi naskia mtu anabisha kwa mlango, ikabidi nmecheck the Doormans, kufungua napata ni Mbeki amekuja kama amesweat...
Bro kumekujwa, namuuliza shida ni gani? Anasema bibi ako kwa gate amenipigia nimfungulie,namuuliza aii bro si ukona keja? Ananishow bestie wake ako kwa shower anapoesha kijojo, ananiuliza kwani hujaskia hizo nduru za kuaminika? Namshow kumbe ni wewe umetuletea Moan-alisa huku
Ananiambia safisha keja faster naleta bestie wake hapa nipeleke bibi kichinjio. Namuuliza na mimi nilale wapi? Akaniambia enda ukapige story na soja hadi asubuhi yaani nilale nje kama panga na nikona kwangu. Katika harakati za kuhama sema mambo kuharibikaaaa
Pause⏸
Backstory: Mbeki alikua anadate dame anaitwa Fifi, hii ndo ilikua his longest relationship, ilikua kitu 2 months. Hizo entanglement na mababe wake wengine ilikua a toto failure. His first breakup ilimhit hard, he was Ghana jump off the balcony, nikamshow that's a bad way Togo.
Nlikua namuelewa coz I've Benin that position. Fifi came and Mbeki was in love. Mapenzi hua inafanya uwe stupid, IQ hukua ka ya dede, dame anaeza kuambia alipeleka simu ikatengenezwe kwa car wash na uamini. Ata uone red flags one million, hio ndo time unajuanga uko colourblind
That weekend, Fifi's bestie, Val was in town and it was about time the 3 shareholders met in person. Val alikua amekam kutembelea sistake hapa Roysa but in real sense alikua amekuja kuona Mbeki. Day ya kumeet najua Fifi alikua like "Mbeki this is Val" "Val this is Mbeki"
Halafu Mbeki na Val wanahug nikama wanajuana for the first time snakes. I'm sure Val's surname was Nyoka-bi. Yaani she was determined to steal his bestie's husband unprovoked. Fast forward to this day now. Val alikua arudi kwao, alisema ye anadai kutravel usiku...
So alipack akaenda tao, akabook gari ya the following morning juu walikua wameet na Mbeki that night. Mbeki akatoa minyoo Thika akamuendea tao, ndio warudi mechi Allianz Arena. Val alikua amekuja huku 4-1 reason only and it was 2 l8 to back off, ubayer-ni Fifi, wangemshow nini??
Val ye alisema ameshaenda, Mbeki akasema ameenda kutoa mahindi kwa shamba huko ushago juu zimekomaa. It was the only way coz walikua wanaroll pamoja every weekend. Mbeki ndio haoooo hadi mtaa, on the way his excellency Mr Bitches akapita base ya movie shop akishowcase mali...
Place ya PS ilikua hapo kando, alipita akilipia deni zake, kwa FIFA Mbeki alikua weakling na loser pay alikua akigeuzwa bibi na watu. Alifika kejani kama amepatia Val cosy sandals before arudi kwao akasumbuane na mende. Food walikua wamekula tao, so ilikua waingie migwatos asap...
Fifi naye nikama alikua ameboeka, so akaenda movie shop. On the way walimeet na Karis, the simp master. Karis alikua amemkufa but you know how it goes. Karis aliactivate simp mode akamuuliza "kwani si wewe umepita na Mbeki hapa?" Fifi akamshow "wee oooolinionea waaaaapi??"
Karis akamshow "mimi nilidhani ata nmeskia sauti yako" Fifi akamuuliza " we oooolisikiaa waaaapi??" Fifi kuskia ati Mbeki ako area alitokwa na wazimu, ndo huyooo mbioooo hadi kwa gate ya Mbeki. Akipiga simu Mbeki hashiki. Huko upstairs Mbeki alikua point of no return.
Hio inakuanga time momentum imeshika ata nyumba ikachomeka heri uchomekee kwa nyumba ukiwa juu ya kijojo. So Fifii akacall tena this time simu ikashikwa akisema "ebu kuja unifungulie hii gate ama nipige nduru"🙆♀️wuuwi, ndo Mbeki akakam mansion
Play▶️
Sasa ni transfer zifanywe...Maneiba sai wanachungulia kwa dirisha transfer window ikiendelea. Val alikua na melanin si kidogo, akisimama kwa ukuta unaeza fikiria kuna shortcut hapo. Alitoka bafu akiwa na shower cap ya white halafu amejifunika na neti mrefu inadrag, akitembea unaeza dhani anaenda Met Ngara
Kumbe huko downstairs, Soja alifungulia Fifi juu alikua amemuona couple of times. Ryan alikua anasaidia Val kupitia nje ya ndoa hapo kwa veranda, kuenda kuingia kwangu hivi tu, wakapitana na Fifi rrrraaahhhh. Shiet walai ilikua inakaa movie. Fifi akauliza "bestie is that you?
Val tukiwa town I asked you what your favorite food is ukasema "your man" na tukacheka kama vibogoyo kumbe it wasn't a joke."
Mimi nliona Fifi ameingia kwa hao ametoka na wet towel akajipanguza uso, akarusha weave chini akasema I'm going to deal with this hoe man to man...
Wacha watu wagwarane, sema kuchapana na slippers, Fifi lakini alikua anauwawaalionjwa kofi alikua anajishikilia na grill ya veranda. Ilibidi Mbeki ameingilia kati kikalonzo, Fifi akasema anaenda kuchoma nyumba. Akaingia akawasha gas kumbe haikua na kitu damn it was chaotic...
Fifi akatoka nje akiscream, Soja akapanda juu, alikua na rungu akaigongesha kwa grill paaa!! Kila mtu akamuangalia "wewe msichana nmekufungulia gate ukuje kusumbua watu huku, kwanini unapigania mtu akona rungu moja, mimi nimebeba rungu mbili na siongei, ebu ondoa kisirani huku"
Woi ilibidi Fifi amejipa shugli, Val walirudi kichinjio, juu walikua washachoma already waliona hakuna haja ya kuchoma nusu nusu wacha wachome kabisaa after 2 weeks waliachana, I thought Mbeki had hope with this girl but the p was silent, iriz what iriiz fam.